Pages

Thursday 18 June 2015

Kiungo wa Chile Arturo Vidal Ameachiliwa na Polisi Baada ya Kukamatwa

Kiungo wa Chile Arturo Vidal ameachiliwa na polisi baada ya kukamatwa kwa kosa la kusababisha ajali kwa madai wa ulevi. Vidal, 28, ambaye ndio anayeongoza kwa kufunga magoli katika michuano ya Copa America 2015 nchini mwake, Chile, alipata ajali na Ferrari yake usiku wa Jumanne. 

Leseni ya kuendesha gari ya Vidal aliyepata majeraha madogo, imesitishwa, lakini ataendelea kichezea Chile. "Nimewaangusha watu wote," alisema Vidal akibubujikwa na machozi baada ya kuachiliwa.

0 comments:

Post a Comment