Pages

Thursday 18 June 2015

Aguero Akitua Madrid Inabidi Benzima Auzwe

Inasemekana kwamba kiwango anachokionyesha Sergio Aguero kwenye michuoano ya Copa Amerika kimewavutia mabosi wa Real Madrid na kushwawishika kutaka kusajili ndani ya klabu hiyo tajiri dunuiani.

Aguero kwa sasa anakipiga ndani ya klabu ya Manchester City ya Uingereza na mkataba wake unamuhitaji awepo ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2019.

Madrid watalazimika kutoa kitika cha dola milioni 50 ili wampate kijana huyo ambaye msimu uliopita alikua mfungaji bora wa ligi ya Uingereza.

Kama hilo likitokea basi moja kwa moja mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema itabidi auzwe kwa maana mfumo wa kocha mpya wa Rafael Benitaz utamuweka Christian Ronald acheze namba tisa ambayo amnaicheza Benzama hivyo ni wazi kwamba Benzema atakaa benchi.

Klabu ya Real Madrid inamtaka mchezajiw a pembeni atakayeweza kucheza namba ya Christian Ronaldo, hivyo ikifanikiwa kuchukua Sergio Aguero ni wazi kwamba itabidi acheze winga ya Ronaldo.

Lakini hata hivyo huwenda hilo lisitokee kwani horodha ya majina kutoka kwa kocha Benitez haionyeshi kwamba jina la Aguero limo.

0 comments:

Post a Comment