Pages

Thursday 18 June 2015

Kadi Nyekundu Yatibua Rekodi Brazili na Colombia

Ni zaidi ya miaka 24 timu ya taifa ya Colombia haijawahi kuifunga timu ya taifa ya Brazili katika mchezo wa soko.

Rekodi hiyo ilivunjwa jana usiku katika mchezo dhidi ya timu hizo mbili kivumbi cha michuano ya kombe Copa Amerika baada ya Wacolombia kuwafunga Wabrazuli kwa bao moja kwa nunge mnamo dadiki ya 36, bao lililowekwa kimiani na mchezaji Jeison Murillo.

Lakini tukio la kushangaza ni kadi mbili walizopata wachezaji Naymar (Brazil) na Carlos Bacca (Colombia) mnamo dakika za mwisho kabisa wakati refarii Enrique Osses Kutoka nchini Chile akipuliza firimbi kuashiria kwamba dakika za mchezo huo zimeisha.

Wakati refarii huyo akipuliza filimbi ya kumaliza mchezo huo, Mchezaj Naymar alipiga shuti kwa hasira na likatua mgongoni mwa mchezaji Carlos Bacca ambapo ilisababisha vurugu kubwa uwanjani hapo.



Wacheazji wa timu zote mbili walivamiana na kufanyiana fujo, kabla ya walinzi, makocha na wachezaji wa akiba kuingilia kati kuamua ugomvi huo.

Refarii Enrique Osses aliwalima kadi wacheazji wote wawili, ambapo sasa watakosa michezo inayofuatia ambapo Brazili siku ya jumapili ijayo itakutana na Venezuela na Colombia watacheza na Peru.

0 comments:

Post a Comment